Philippians 2:6-11


6 aYeye, ingawa alikuwa na asili ya Mungu hasa,
hakuona kule kuwa sawa na Mungu
kuwa kitu cha kushikilia,

7 bbali alijifanya si kitu,
akachukua hali hasa na mtumwa,
naye akazaliwa katika umbo la mwanadamu.

8 cNaye akiwa na umbo la mwanadamu,
alijinyenyekeza, akatii hata mauti:
naam, mauti ya msalaba!

9 dKwa hiyo, Mungu alimtukuza juu sana,
na kumpa Jina lililo kuu kuliko kila jina,

10 eili kwa Jina la Isa, kila goti lipigwe,
la vitu vya mbinguni, na vya duniani,
na vya chini ya nchi,

11 fna kila ulimi ukiri ya kwamba
Isa Al-Masihi ni Bwana,
kwa utukufu wa Mungu Baba.

Ng’aeni Kama Mianga Katika Ulimwengu

Copyright information for SwhKC